Mbunge wa zamani wa Ukraine auwawa Uhispania
21 Mei 2025Haya yamesemwa na chanzo kimoja cha polisi ya Uhispania. Vyombo vya habari vya Uhispania vimesema Andriy Portnov alikuwa ametoka kuwapeleka wanawe shule ndipo alipouwawa kabla ya kuingia kwenye gari lake.
Portnov alikuwa mbunge nchini Ukraine katika miaka ya 2000 na akawa naibu mkuu wa utawala wa rais chini ya Yanukovich kabla ya kukimbilia Urusi mwaka 2014 baada ya kuamrisha kushambuliwa kwa waandamanaji wa Ukraine waliokuwa wanataka kujiunga na Umoja wa Ulaya.
Marekani ilimuwekea vikwazo mwaka 2021 kutokana na madai ya ufisadi. Mamlaka nchini Ukraine hazijatoa tamko lolote kuhusu tukio hilo ila nchi hiyo imehusishwa na mauaji kadhaa nchini Urusi na maeneo ya Ukraine yanayokaliwa na Urusi, tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi mwaka 2022.
Mauaji ayo yamekuwa yakiwalenga maafisa wa kisiasa, kijeshi au wanaounga mkono vita vya Ukraine.