Mbappe atarajiwa kukosa mechi dhidi ya Pachuca
22 Juni 2025Matangazo
Kwa mujibu wa msemaji wa Real Madrid, KylianMbappé hakushiriki mazoezi ya pamoja na huenda atakosa mechi hiyo ya kundi H baada ya kulazwa hospitali kutokana na maumivu ya tumbo mapema wiki hii.
Nyota huyo pia alikosa mechi ya ufunguzi ya Real dhidi ya Al-Hilal, iliyomalizika kwa sare ya 1-1. Matokeo yaliyoipa nafasi RB Salzburg kuongoza kundi H kwa alama tatu baada ya kuwafunga Pachuca ya Mexico kwa mabao 2-1.
Katika mechi nyengine Juventus watavaana Wydad ya Moroko na hapo kesho Manchester City itakipiga na Al Ain huku RB Salzburg ikitarajia kucheza na Al-Hilal.