Mazungumzo ya wajumbe wa Ukraine na Urusi yamalizika
2 Juni 2025Matangazo
Duru ya pili ya mazungumzo ya moja kwa moja kati ya wajumbe wa Urusi na Ukraine imemalizika baada ya muda wa saa moja, kwa mujibu wa shirika la habari la Urusi na rais Volodymyr Zelensky.
Mazungumzo hayo yaliyofanyika Istanbul nchini Uturuki hayakuwekewa matumaini makubwa kufuatia msururu wa mashambulizi ya Ukraine dhidi ya Urusi yaliyotokea mwishoni mwa Juma.
Hata hivyo rais Zelensky akizungumza kutokea Vilnius,Lithuania amesema kufuatia mkutano huo,hatua nyingine ya kuachiliwa wafungwa wa kivita inaandaliwa.