Mazungumzo ya utekelezaji mkataba wa amani kati ya serikali ya Burundi na FNL
8 Mei 2007
Mpatanishi wa mazungumzo ya utekelezaji mkataba wa amani nchini Burundi kati ya serikali na kundi la mwisho la waasi FNL, Waziri wa ndani wa Afrika kusini Bw.Charles Ncgakula anatazamiwa kuwasili Burundi,lengo la kuyafufua mazungumzo yaliokwama kati ya pande hizo mbili, ya ile tume ya kusimamia utekelezaji wa usimamishaji mapigano.
Hali hiyo imezuka baada ya FNL kudai ufafanuzi ni nyadhifa gani watakazopewa serikalini na katika taasisi za dola, wakati Rais Pierre Nkurunziza kuwashutumu wajumbe wa FNL kwa kile alichokiita "kutoa madai mapya kila mara".
Mwandishi wetu mjini Bujumbura Amida Issa ana ripoti kamili.