Mazungumzo ya UN kuhusu mkataba wa plastiki yarefushwa
15 Agosti 2025Mazungumzo ya kusaka mkataba wa kimataifa wa kupambana na uchafuzi wa plastiki duniani, yanayofanyika Geneva nchini Uswisi yamerefushwa baada ya kufikia muda wa mwisho bila maelewano.
Angalau nchi zipatazo 180 zinakubaliana kwamba uchafuzi wa plastiki duniani unatoa kitisho kikubwa, lakini bado zinatofautiana katika masuala kadha.
Zaidi ya wanachama 100, ikiwa ni pamoja na Umoja wa Ulaya na mataifa kadhaa ya Amerika Kusini, Afrika na Asia, yanashinikiza kuwepo na ukomo wa uzalishaji plastiki duniani.
Mataifa yanayozalisha mafuta yanapinga suala la ukomo wa uzalishaji plastiki zitokanazo na mafuta ya petroli, makaa ya mawe na gesi.Mazungumzo ya mkataba wa plastiki yaendelea Geneva
Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo OECD limeonya kwamba ikiwa hatua hazitochukuliwa haraka, uzalishaji wa plasitiki utaongezeka mara tatu kufikia mwaka 2060 na kuathiri zaidi dunia na binadamu.