Mazungumzo ya mkataba wa uchafuzi wa plastiki yakwama
14 Agosti 2025Matangazo
Hatua huiyo imeyaacha mazungumzo hayo katika hali ya sintofahamu.
Wakati muda wa kusaini makubaliano ukiendelea kuyoyoma baadhi ya mataifa kati ya nchi 184 zilizokusanyika kwenye ukumbi wa Umoja wa Mataifa huko mjini Geneva, zimelaumu maandishi yaliyopendekezwa ya maelewano ambayo yametolewa na mwenyekiti wa mazungumzo hayo Luis Vayas Valdivieso wa Ecuador.
Nchi hizo zinataka kuchukuliwe hatua kabambe kwa kile wanachokiona kuwa ni upungufu wa hatua kali za kisheria, zikisema maandishi ya rasimu hiyo ni ya chini kabisa na kuyafanya makubaliano juu ya usimamizi wa taka kuwa dhaifu.