SiasaSudan
Mazungumzo ya kutafuta amani Sudan yafanyika London
15 Aprili 2025Matangazo
Mkutano huo unafanyika wakati ambapo umetimia mwaka wa pili wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan. Hata hivyo mazungumzo hayo yanafanyika bila ya ushiriki wa wajumbe wa pande zinazopigana za jeshi la serikali na kundi la RSF.
Mgogoro huo uliozuka miaka miwili iliyopita kati ya majenerali wanaopigania madaraka, unaoitwa na Umoja wa Mataifa kuwa "vita vilivyosahaulika", umesababisha vifo, maafa ya njaa na wakimbizi. Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza David Lammy amesema mkutano huo unaileta pamoja jumuiya ya kimataifa ili kukubaliana juu ya kutafuta njia ya kukomesha mateso kwa watu wa Sudan.
Wajumbe kutoka Ujerumani, Ufaransa,Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika pia wanashiriki kwenye mazungumzo hayo ya mjini London.