MigogoroJamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Mazungumzo kati ya serikali ya DRC na M23 kufanyika Luanda
12 Machi 2025Matangazo
Taarifa imesema Angola "kama mpatanishi katika mzozo, itawasiliana na M23 ili kuwakutanisha wajumbe wa Kongo na M23 kwa ajili ya mazungumzo hayo katika siku zijazo ili kupatikane amani ya uhakika.
Hii ni baada ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi nchini Angola, ambapo alijadiliana na Rais Joao Lorenco juu ya mzozo wa mashariki ya Kongo.
Msemaji wa Tshisekedi, Tina Salama, alisema kwenye mtandao wa X kwamba serikali yake itasubiri kuona utekelezaji wa mbinu hii ya upatanishi wa Angola.
Mazungumzo ya amani yamekwama kutokana na Tshisekedi kukataa mara kwa mara kushiriki mazungumzo na M23 wanaoungwa mkono na Rwanda.