MAZOWEZI YA KIJESHI IRAN
20 Agosti 2006Matangazo
TEHERAN:
Kituo cha TV cha Iran kimetangaza kwamba jeshi la Iran limefyatua makombora na yatafanya majaribio ya makombora yanayotoka ardhini kwenda baharini wakati wa mazowezi ya kijeshi yanayoendelea wakati huu.
Jeshi la Iran lilianza jana mazowezi kusini mwa Iran na kuarifu kwamba, zana mpya za kijeshi za kiiran zitajaribiwa.