Mawaziria mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wajadili uhamiaji
23 Julai 2025Mawaziri wa mambo ya ndani wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya wanakutana Copenhagen, mji mkuu wa Denmark kujadili njia za kuongeza safari za kurejesha makwao raia wa mataifa ya kigeni.
Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Alexander Donbrindt amependekeza kwamba kundi dogo la nchi za Umoja wa Ulaya huenda zikaungana kuanzisha vituo vya kuwapokea waomba hifadhi watakaokataliwa katika nchi zilizo nje ya Umoja wa Ulaya.
Pamoja na suala la kuwarejesha wahamia waliokataliwa maombi yao katika nchi zao wanakotokea, mazungumzo ya Copenhagen yanatuwama juu ya hatua dhidi ya uhamiaji usio na mpangilio na mapambano dhidi ya uhalifu wa kupanga na ulanguzi wa dawa za kulevya.
Nchi wanachama pia zinapania kuwa na jukumu kubwa na imara zaidi kwa wakala wa ulinzi wa mipaka Frontex.