Mawaziri wawili wa Ghana wauwawa katika ajali ya helikopta
7 Agosti 2025Matangazo
Ofisi ya rais wa Ghana John Mahama imesema mawaziri hao walikufa baada ya helikopta ya jeshi la anga iliyokuwa imewabeba wafanyakazi watatu na abiria watano kuanguka katika msitu kusini mwa nchi hiyo.
Kituo cha televisheni cha Joy News kilionyesha mkanda wa video iliyorekodiwa na simu ya mkononi kutoka eneo la ajali ikionyesha mabaki ya ndege yakiwaka moto na kufuka moshi katika eneo la msitu mkubwa mapema jana kabla kufichuliwa kwamba mawaziri hao walikuwa miongoni mwa waliokufa.
Boamah alikuwa waziri wa ulinzi muda mfupi baada ya rais Mahama kuapishwa Januari mwaka huu.