Mawaziri wajiuzulu Chad kwa video ya ngono
18 Oktoba 2023Matangazo
Waziri wa Ulinzi, Daoud Yaya Brahim, na Katibu wa Serikali, Haliki Choua Mahamat, walijiuzulu siku ya Jumatano (Oktoba 18) baada ya mikanda miwili tofauti ya video inayowaonesha viongozi hao wakifanya mapenzi na watu wengine.
Video hizo zilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii Jumapili iliyopita.
Soma zaidi: Chad kuwasindikiza wanajeshi wa Ufaransa kutoka Niger
Kwa mujibu wa msemaji wa serikali ya Chad, Waziri Mkuu Saleh Kebzabo amekubali kujiuzulu kwao.
Hata hivyo, ofisi ya msemaji wa waziri mkuu haikutoa maelezo yoyote.
Shirika la habari la Reuters halikuweza kuwapata mara moja viongozi hao watoe kauli zao.