Mawaziri wa EU wakutana kuzijadili Ukraine na Gaza
29 Agosti 2025Matangazo
Mazungumzo ya mawaziri wa ulinzi katika siku ya kwanza ya mkutano yatajadili kuiunga mkono Kyiv na kuimarisha ushirikiano na sekta ya Ulinzi ya Ukraine. Mkuu wa sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya Kaja Kallas kabla ya kuanza kwa mkutano amesisitiza juu ya umuhimu wa kuendelea kuisaidia Ukraine.
Mawaziri wa mambo ya kigeni watakaokutana Jumamosi wanatazamiwa kumshinikiza Rais wa Urusi Vladimir Putin akubali kusitisha vita. Pia watajadili kuhusu hali ya Ukanda wa Gaza wakati mataifa wanachama wa Umoja huo yakikabiliwa na mgawanyiko kuhusu hatua za Israel katika Ukanda huo.