Mawaziri wa mambo ya ndani wa EU wajadili uhamiaji
22 Julai 2025Matangazo
Mawaziri wa mambo ya ndani wa Umoja wa Ulaya, wanakutana mjini Copenhagen nchini Denmark kujadili kuhusu hatua za pamoja, kudhibiti uhamiaji usiofuata sheria, kupambana na uhalifu wa kupanga na biashara ya mihadarati.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa UjerumaniAlexander Dobrindt, amedokeza kwamba mataifa kadhaa ya Umoja huo huenda yakaungana kujenga katika mataifa ya nje ya Ulaya, vituo vya kuwaweka wahamiaji walionyimwa hifadhi ya ukimbizi.
Lengo la hatua hiyo ni kuwarejesha haraka katika mataifa walikotokea, waomba hifadhi walioingia barani Ulaya.
Mbali na uhamiaji mawaziri hao watajadili pia kuhusu namna Umoja wa Ulaya unavyoweza kuwa tayari kuikabili migogoro ikiwemo majanga ya kiasili au kuporomoka kwa mifumo ya mawasiliano.