Mawaziri wa G20 wakutana Afrika Kusini bila Marekani
20 Februari 2025Matangazo
Hata hivyo, mkutano huo umegubikwa na hatua ya kutohudhuria Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio ambaye ameikosoa Afrika Kusini kwa kuendesha ajenda ya kuipinga Marekani.
Mkutano huo wa siku mbili, unaofanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika, ni wa matayarisho ya mkutano wa kilele wa viongozi wa kundi hilo utakaofanyika mwezi Novemba.
Soma pia:Trump amuita Zelensky "Dikteta ambaye hakuchaguliwa"
Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ambaye ndiye mwenyekiti wa sasa wa G20, anatarajiwa kutoa hotuba yake ya ufunguzi mchana huu. Vita na migogoro barani Afrika na Ulaya ndio ajenda kuu itakayoutawala mkutano huo.