Mawaziri wa Israel kuamua iwapo wataimarisha vita Gaza
4 Mei 2025Matangazo
Hayo yanajiri wakati ambapo jeshi limeanza kuwaita maelfu ya askari wa akiba ili kuupanua wigo wa mashambulizi. Wakati huo huo shambulio la kombora lililofanywa na waasi wa Yemen wanaoungwa mkono na Iran limesababisha usafiri wa ndege katika uwanja mkuu wa ndege wa Israel kusimamishwa.
Mipango ya kuzidisha mashambulio kwenye Ukanda wa Gaza , baada ya zaidi ya miezi 18 ya vita, inafanyika wakati maafa yanazidi kuwa makubwa kwa Wapalestina.
Tangu mwezi Machi Israel imezuia misaada ya chakula kuingia kwenye Ukanda wa Gaza ili kuwashinikiza Hamas wakubali mazungumzo kwa masharti yao. Kutokana na hali hiyo watu milioni 2.3 wa Gaza wanakabaliwa na masaibu makubwa kabisa tangu kuanza kwa vita.