Mawaziri wa G7 wajadili usitishaji mapigano Ukraine
13 Machi 2025Matangazo
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio anatarajiwa kuwasilisha kwenye mkutano huo juhudi zinazoongozwa na nchi yake za kutafuta usitishaji vita vya miaka mitatu nchini Ukraine vilivyosababisha umwagaji damu mkubwa.
Soma pia:Mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la G7 wakutana nchini Japan
Mkutano huo unakuja baada ya waziri huyo kukutana na wajumbe wa Kiev mjini Jeddah Saudi Arabia mwanzoni mwa wiki hii.Aidha akiwasili jana katika mji wa Charlevoix kutakakofanyika mkutano huo, Rubio alisema mkutano huo sio wa kujadili namna Marekani itakavyoichukuwa Canada.