Mawaziri wa fedha wa G7 wapuuza ushuru wa Trump
22 Mei 2025Matangazo
Mawaziri wa fedha kutoka mataifa tajiri kiviwanda duniani ya kundi laG7 wamepuuza mvutano uliosababishwa na hatua ya rais Donald Trump ya kutangaza ushuru wa ziada.
Viongozi hao waliokutana jana huko Banff nchini Canada, badala yake wametafuta msimamo wa pamoja kuhakikisha mkutano huo unafanikiwa kupata makubaliano kuhusu tamko la pamoja ambalo halikugusia suala hilo la ushuru.
Miongoni mwa masuala yaliyojadiliwa na viongozi hao, ni pamoja na hatua ya kuiunga mkono Ukraine, vitisho vya mataifa kama China pamoja na namna ya kukabiliana na uhalifu wa kifedha na biashara ya mihadarati.