Mawaziri wa biashara wa EU kuijibu Marekani kuhusu ushuru
7 Aprili 2025Matangazo
Mawaziri wa biashara wa nchi za Umoja wa Ulaya wanakutana Luxembourg leo Jumatatu kuweka mikakati ya kumshawishi rais wa Marekani Donald Trump kuondowa ushuru aliouwekea Umoja huo.
Mawaziri hao wa biashara wanatarajiwa pia kujadili ushuru inaoweza kuupitisha kuijibu Marekani pamoja na kuchukuwa hatua nyingine za kulipiza,ambazo zinaweza kutekelezwa ikiwa juhudi za mazungumzo ya kutafuta suluhu na Marekani hazitofanikiwa.Mataifa 50 yasaka mazungumzo na kibiashara na Marekani kuhusu ushuru wa Trump
Bidhaa kutoka mataifa ya Umoja wa Ulaya zinakabiliwa na ushuru mpya wa asilimia 20 kuanzia Jumatano. Mataifa mengi ya jumuiya hiyo yanakhofia viwango hivyo vipya vya ushuru vitakuwa na athari kubwa kwa mataifa ya dunia.