JangaAsia
Matumaini ya kuwapata manusura Afghanistan yafifia
3 Septemba 2025Matangazo
Shirika la Kimataifa la Save the Children limesema moja ya timu zake za uokoaji imelazimika kutembea umbali wa kilometa 20 kuvifikia vijiji vilivyopoteza mawasiliano kutokana na miamba iliyoanguka, wakiwa wamebeba vifaa vyao migongoni. Shirika la Afya duniani WHO limeonya kuwa idadi ya majeruhi watetemeko hilo la ardhi inatarajiwa kuongezeka kwa kuwa bado kuna watu wengi walionasa ndani ya majengo yaliyoporomoka. Mamlaka za ndani zinasema wengi wa waathiriwa walioko chini ya vifusi wako katika wilaya ya Nurgal mkoa wa Kunar. Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.0 kwa kipimo cha richta liliikumba Afghanistan usiku wa kuamkia Jumapili ambapo hadi sasa zaidi ya watu 1,400 wamekufa na zaidi ya 3,300 wamejeruhiwa.