MigogoroMashariki ya Kati
Matumaini bado madogo usitishaji vita Ukanda wa Gaza
15 Julai 2025Matangazo
Mazungumzo hayo yanayoendelea mjini Doha, Qatar yameshuhudia kila upande ukiulamu mwingine kuwa chanzo cha mkwamo wa kupatikana mkataba wa usitishaji vita kwa muda wa siku 60.
Kundi la Hamas hapo jana limemtuhumu Waziri mKuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuwa sababu ya kutofikiwa makubaliano likisema kiongozi huyo anacho "kipaji cha kuvuruga kila mchakato wa usuluhishi".
Netanyahu amesema hatokubali kuvimaliza vita vya Gaza hadi kundi la Hamas likubali kuweka chini silaha na lisiwe na jukumu lolote la uongozi kwenye ardhi hiyo ndogo ya Wapalestina.
Wapatanishi wamesema wanatumia kila njia kumaliza tofauti kubwa ya misimamo iliyopo kati ya pande hizo mbili ili makubaliano yafikiwe haraka iwezekanavyo.