Matokeo ya Uchaguzi wa Ujerumani katika michoro
23 Februari 2025Kwa idadi ya wapiga kura ya rekodi ya asilimia 83.5, kiwango cha juu zaidi tangu 1990, Wajerumani walipiga kura katika uchaguzi wa mapema wa shirikisho mnamo Februari 23. Uchaguzi huu uliitishwa baada ya serikali ya muungano wa vyama vitatu—Social Democrats (SPD), Chama cha Kijani, na chama cha kiliberali cha Free Democratic Party (FDP)—kuporomoka mwishoni mwa mwaka 2024.
Kura za vyama katika uchaguzi wa bunge la Ujerumani
Kulingana na makadirio, Chama cha kihafidhina cha Christian Democratic Union (CDU) kinachoongozwa na mgombea wa ukansela Friedrich Merz na chama ndugu, Christian Social Union (CSU), kimepata kura nyingi zaidi, kikifuatiwa na chama cha mrengo mkali wa kulia cha Alternative for Germany (AfD).
Mafanikio na hasara za vyama vya siasa vya Ujerumani
Mshindi mkubwa wa uchaguzi kwa upande wa mgao wa kura ni chama cha mrengo mkali wa kulia, AfD, huku SPD inayoongozwa na Kansela Olaf Scholz ikiandikisha hasara kubwa zaidi ya kura ikilinganishwa na uchaguzi uliopita.
Viti vinagawanywaje katika bunge la Ujerumani?
Kuna viti 630 katika Bundestag, bunge la Ujerumani. Idadi ya viti ambavyo chama kinapata inategemea mgao wa kura zao. Chama lazima kipate angalau asilimia 5 ya kura ili kuingia bungeni.
Vyama vinavyoweza kuunda muungano wa serikali
Ingawa CDU/CSU wamepata asilimia kubwa zaidi ya kura, hawana wingi wa moja kwa moja. Watalazimika kuunda muungano na chama kingine ili kupata viti 316 katika Bundestag na kuunda serikali ijayo. Kikokotoo cha muungano kinaonyesha ni mchanganyiko upi wa vyama unaowezekana kulingana na mgao wao wa kura.
Uhamaji wa wapiga kura
Uchaguzi wa Jumapili ulishuhudia wapiga kura wakibadili uaminifu wao wa kisiasa na kuhama kati ya vyama. Moja ya mabadiliko makubwa zaidi ilikuwa kuhama kwa wapiga kura kutoka chama cha SPD, kwenda muungano wa kihafidhina wa CDU/CSU, ambao umeongeza takriban kura milioni 2 kutoka kwa wa Social Democrat. Chama cha Die Linke pia kilinufaika na uhamaji wa wapiga kura kutoka SPD na Kijani, kikiongeza kura 540,000 kutoka SPD na 600,000 kutoka Kijani.