MigogoroMashariki ya Kati
Mateka watatu wa Israel waachiliwa huru na kundi la Hamas
1 Februari 2025Matangazo
Yarden Bibas mwenye miaka 35 na Ofer Calderon mwenye miaka 54 wameachiliwa huru mapema leo na kukabidhiwa kwa Shirika la msalaba mwekundu katika mji wa Khan Younis wakati Keith Siegel mwenye uraia pacha wa Israel na Marekani akikabidhiwa kwa shirika hilo katikakati mwa Gaza.
Soma zaidi: Israel na Hamas zabadilishana wafungwa kwa mateka
Israel tayari imethibitisha kuwapokea Calderos na Bibas. Kama sehemu ya makubaliano, baadaye Jumamosi Israel inatazamiwa kuwaachilia wafungwa 183 wa Kipalestina.
Hadi sasa mateka 18 wa Israel waliokuwa wakishikiliwa na wanamgambo wa Hamas na mamia ya wafungwa wa Palestina waliokuwa katika jela za Israel wameachiliwa huru katika kipindi cha wiki mbili tangu makubaliano ya kusitisha vita yalipoanza kutekelezwa.