MigogoroMashariki ya Kati
Mateka 3 wa Israel, wafungwa 183 wa Palestina waachiwa huru
8 Februari 2025Matangazo
Watu hao Eli Sharabi, Or Levy na Ohad Ben Ami, wamekuwa wakishikiliwa mateka huko Gaza kwa miezi 16 na wameachiliwa kama sehemu ya makubaliano ya usitishaji mapigano kati ya Israel na Hamas huko Gaza.
Hatua hii ya leo imewezesha pia kuachiliwa kwa wafungwa 183 wa Kipalestina waliokuwa wakishikiliwa katika gereza za Israel na ambao tayari wamewasili mjini Ramallah.
Tangu kuanza kutekelezwa kwa makubaliano hayo Januari 19 mwaka huu, Hamas imewaachia mateka 13 wa Israel na raia watano wa Thailand huku Israel ikiwaachia wafungwa 583 wa Kipalestina.