Shirika la utangazaji la serikali nchini China CCTV, lasema serikali ya nchi hiyo kuzisaidia kampuni zinazotengeza bidhaa muhimu kurejea kazini haraka iwezekanavyo, mamia ya raia wa Lebanon na Palestina waandamana leo karibu na ubalozi wa Marekani nchini Lebanon na waziri wa ulinzi wa Ufaransa Florence Parly, asema taifa hilo litawapeleka wanajeshi mia sita zaidi katika eneo la Sahel, Afrika.