Rais wa Rwanda Paul Kagame ameapishwa Jumapili 11/08/24 kuhudumu muhula wa nne madarakani. Mamia ya Wapalestina wakimbia makaazi yao baada ya jeshi la Israel kuwaamuru waondoke Khan Younis. Urusi yakiri kuwa vikosi vya Ukraine vimefanya mashambulio ndani ya ardhi ya Urusi. Zaidi ya watu 10 wafariki baada ya mrundo wa taka kuporomoka mjini Kampala.