SiasaAsia
Mataifa masikini yakabiliwa na wimbi madeni ya China
27 Mei 2025Matangazo
Taasisi ya Lowly inayofuatilia kiwango cha madeni ulimwenguni imesema mradi wa miundombinu wa China, maarufu kama BRI, uliotowa mikopo mikubwa kwa ajli ya ujezi wa bandari, reli, barabara na majengo katika mataifa ya Afrika, Asia na Pasifiki, umesababisha kiwango kikubwa cha madeni kwa mataifa hayo yanayoendelea.
Soma zaidi: Kongamano la China- Afrika kuja na matokeo yenye tija?
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, ndani ya muongo huu, China itakuwa mnufaika mkubwa wa kukusanya madeni yake badala ya kuwa muwekezaji kwenye mataifa hayo, huku nchi zilizokopeshwa zikiingia kwenye wimbi kubwa la ufukara kutokana na kulipa madeni hayo.