Mataifa ya Ulaya yatishia kuongeza vikwazo dhidi ya Urusi
13 Mei 2025Wanadiplomasia hao wameituhumu Ikulu ya Kremlin kwa kile walichokiita "kufanya michezo” kuhusu mazungumzo ya amani na Ukraine.
Katika taarifa ya pamoja baada ya mkutano wao katika mji mkuu wa Uingereza, mawaziri hao wa mambo ya nje wameeleza wasiwasi wao kwamba Urusi "haijaonyesha nia ya dhati ya kupiga hatua.”
Soma pia: Marekani, UK zaahidi jibu la haraka kwa maombi ya Ukraine
Mawaziri hao kutoka Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Poland, Uhispania na Umoja wa Ulaya wamesema katika tamko la pamoja, kwamba "Urusi lazima ikubali mpango wa kusitisha mapigano bila kuchelewa.”
Moscow kwa upande wake imepuuzilia mbali shinikizo kutoka kwa viongozi wa Ulaya la kuitaka kuukubali mpango wa kusitisha mapigano kwa siku 30 bila masharti yoyote kuanzia jana Jumatatu, ikisema Urusi haitakubali vitisho.