Ujerumani, Ufaransa, Uingereza kupeleka mawaziri wake Gaza
29 Julai 2025Matangazo
Merz ameitoa kauli hiyo wakati shinikizo likiongezeka kuhusu hali mbali ya kiutu kwenye ukanda huo. Kansela Meru ameyasema hayo mjini Berlin mbele ya waandishi wa habari akiwa na Mfalme wa Jordan Abdullah II aliye ziarani Ujerumani. Ameongeza kuwa nchi hizo tatu zinaamini serikali ya Israel iko tayari kutambua kuwa hatua zinapaswa kuchukuliwa kukabiliana na hali ya sasa.
Ujerumani ambayo siku zote imekuwa upande wa Israel, ikiwa na Ufaransa na Uingereza zimeongeza miito ya kuitaka Israel kuruhusu misaada ya kiutu iingizwe Gaza mahali ambako Israel inapambana kulisambaratisha kundi la Hamas. Wiki iliyopita nchi hizo zilitoa taarifa ya pamoja zikitaka janga la kiutu Ukanda wa Gaza lifike mwisho.