MigogoroMashariki ya Kati
Mataifa ya Kiarabu yapitisha wazo la Misri la ujenzi wa Gaza
5 Machi 2025Matangazo
Pendekezo hilo ni tofauti na maono ya Rais wa Marekani Donald Trump ya kutengeneza kile alichokiita "Eneo la mapumziko la Mashariki ya Kati".
Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sissiamesema pendekezo hilo, lililokaribishwa na Hamas na kukosolewa na Israel, limekubaliwa wakati wa kuufunga mkutano wa kilele wa Cairo Jumanne.
Sisi amesema Misri imeshirikiana na Wapalestina katika kuunda kamati ya utawala ya watalaamu wa Kipalestina walio huru watakaokabidhiwa utawala wa Gaza baada ya kumalizika kwa vita.
Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas amelikaribisha pendekezo hilo la Misri na kumuomba Rais wa Marekani Donald Trump kuunga mkono mpango wa aina hiyo ambao hautahusisha kuwahamisha wakaazi wa Kipalestina.