MigogoroMashariki ya Kati
Gaza: Nchi za Kiarabu na Kiislamu zalaani mpango wa Israel
9 Agosti 2025Matangazo
Nchi karibu 20 za Kiarabu na Kiislamu ikiwa ni pamoja na Misri, Saudi Arabia na Uturuki, zimesema mpango huo wa kuchukua udhibiti wa Gaza City ni "ukiukwaji wa wazi wa sheria za kimataifa, na jaribio la kulazimisha na kuimarisha ukaliaji haramu".
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini El Alamein baada ya kukutana na Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan amesema ni lazima nchi za kiislamu ziwe na umoja ulio thabiti pamoja na kuhamasisha jumuiya ya kimataifa ili kupinga mpango huo wa Israel wa kutaka kuudhibiti mji wa Gaza.