MigogoroMashariki ya Kati
Nchi za G7 zataka mateka waachiliwe, misaada iingie Gaza
15 Machi 2025Matangazo
Wito huo umetolewa katika kauli ya pamoja iliyotolewa Ijumaa baada ya mkutano wao nchini Canada.
Kundi hilo linaloundwa na mataifa ya Canada, Marekani, Uingereza, Ufaransa, Italia na Japanzimetaka pia miili ya waliouwawa katika mzozo huo wa Mashariki ya Kati irejeshwe nyumbani.
Soma zaidi: Mawaziri wa G7 wakutana kujadili mzozo wa Gaza na Ukraine
Kando ya hayo, mawaziri hao wa mambo ya kigeni wa G7 wametoa wito wa misaada ya kiutu kuruhusiwa kuingia Gaza bila vikwazo baada ya Israel kusitisha misaada kufikishwa kwenye ukanda huo.
Wametaka pia kuwe na makubaliano ya kudumu ya kuvimaliza vita katika mzozo huo wa Mashariki ya Kati huku wakisema kuwa ongezeko la mivutano katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu linatia wasiwasi.