Wakuu wa nchi 50 Afrika wakutana Tanzania kujadili nishati
28 Januari 2025Matangazo
Ajenda kuu ya mkutano huo uliopewa jina "Misheni 300", ni upatikanaji wa fedha karibu dola bilioni 90 zitakaowezesha upatikanaji wa nishati ya umeme kwa watu milioni 300 barani afrika kufikia mwaka 2030.
Jana mawaziri walijadili changamoto za upatikanaji wa umeme barani Afrika na leo hii, marais hao wa Afrika wanatarajiwa kusaini mkataba muhimu wa kuwezesha upatikanaji wa umeme kwa wote, katika kipindi ambacho dunia inasisitiza matumizi ya nishati safi ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Takwimu za nishati barani Afrika zinaonyesha kuwa hadi mwaka 2022, asilimia 83 ya watu milioni 685 walikuwa bado hawajafikiwa na nishati ya umeme.