Mataifa ya Afrika Mashariki yapambana kufuzu Kombe la Dunia
26 Machi 2025Tanzania imepata pigo baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka Morocco, ambao sasa wanaongoza kundi E wakiwa na ushindi wa mechi zote tano.
Kenya pia imepoteza mchezo wake dhidi ya Gabon kwa mabao 2-1, huku Pierre-Emerick Aubameyang akifunga mara mbili kuiweka Gabon katika nafasi nzuri kwenye kundi F, nyuma ya Ivory Coast.
Soma pia: Tanzania, Kongo kutupa karata ya kwanza AFCON
Sudan Kusini imefanikiwa kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya majirani zao Sudan, bao la kusawazisha likifungwa dakika za nyongeza na David Sebit, hatua iliyosababisha Sudan kushuka hadi nafasi ya tatu kwenye kundi B nyuma ya Congo na Senegal.
Uganda nayo imeendelea na matokeo mazuri baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Guinea, na hivyo kuimarisha matumaini yao katika kundi G linaloongozwa na Algeria.